MSHAMBULIAJI wa Brazil, Hulk
amethibitisha Jose Mourinho anamtaka Stamford Bridge na ametoa ofa ya
Pauni Milioni 35 kumng'oa Zenit St Petersburg.
Zenit kwa sasa imeichunia ofa ya Chelsea
na wanataka kiasi cha karibu Pauni Milioni 50 walizolipa kwa Porto
kumpata mshambuliaji huyo mwenye kasi msimu uliopita.
Hulk anataka kuondoka Urusi na
anahusishwa na kuungana na Mourinho na aliweka wazi hilo mbele ya
Waandishi wa Habari kwamba anajua Chelsea wametoa ofa kwa ajili yake.

Anayetakiwa: Hulk (kulia) anatakiwa na kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho
Alipoulizwa kuhusu hilo na Waandishi
nchini Brazil jana mchana, alijibu: "Ikiwa nitasema hakukuwa na kitu juu
ya hili, nitakuwa nadanganya. Lakini hiyo si kwa sasa. Kwa sasa, Kwa
asilimia 100 akili yangu nimeielekeza Selecao (Kireno, maana yake timu
ya taifa ya Brazil), na natumaini nitakuwepo na kushinda na timu yangu
kwenye Kombe la Mabara.
"Ni jambo la kujivunia mno kwangu
kucheza nimevaa jezi za njano, karibu mno na familia yangu. Matatizo
mengine itabidi yasubiri hadi wakati wake utakapofika.
No comments:
Post a Comment