IGP MWEMA AFANYA MABADILIKO KWA MAKAMANDA WA MIKOA
Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Said
Mwema, leo amefanya mabadiliko
ya makamanda na wakuu wa
upelelezi katika baadhi ya mikoa
hapa nchini.
Katika mabadiliko hayo aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)
Michael Kamhanda amehamishiwa
Makao Makuu ya Polisi na nafasi
yake inachukuliwa na Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani
Mungi ambae alikuwa Makao
Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya
Jinai.
Aidha, DCP Ally Mlege aliyekuwa
Makao Makuu ya Polisi
amehamishiwa Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu
wa utawala na raslimali watu.
Vilevile, Kamanda wa Polisi mkoa
wa Kipolisi Kinondoni, Charles
Kenyela amehamishiwa Makao
Makuu ya Upelelezi wa makosa ya
jinai -na nafasi yake inachukuliwa
na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa
makosa ya jinai mkoa wa Arusha
ACP Camilius Wambura. Aidha, ACP
Duwan Nyanda aliyekuwa Makao
Makuu ya Upelelezi anaenda kuwa
Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya
jinai Mkoa wa Arusha.
Uhamisho huo ni wakawaida kwa
mujibu wa kanuni, taratibu na
miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
No comments:
Post a Comment