
Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), imeziteuwa timu ya Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), Elect Sports ya Chad na Rayon Sports ya Rwanda kuziba nafasi ya timu za Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Kagame inayoanza Juni 18-Julai 2, Sudan.
Simba, Yanga na Falcon ya Zanzibar hazitashiriki
michuano hiyo kwa maagizo ya serikali kutokana na mashaka ya usalama
nchini Sudan hasa kwenye Jimbo la Darfur ambalo ni moja ya kituo cha
mashindano.
Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholaus Musonye alisema
kujiondoka kwa timu za Tanzania, kusingekuwa mwisho wa mashindano hayo
kwa vile baraza hilo lina timu nyingi.
“Tumeziteua timu hizi baada ya ushawishi wetu kwa
timu za Tanzania kushiriki kushindikana,” alisema Musonye na kuongeza
sababu zilizotajwa na Tanzania kutokushiriki michuano hiyo hazina
mashiko.
Alisema wanatarajia kupanga upya ratiba ya
michuano hiyo katika mkutano wa wajumbe wa Cecafa na waandaaji
utakaofanyika mjini Khartoum.
Musonye alilaumu mwingilio wa mashindano hayo na mambo ya siasa kama ilivyotokea mwaka huu.
No comments:
Post a Comment