Andre Villas-Boas amesema ikiwa klabu ya Tottenham
inataka kufanya vyema msimu ujao basi lazima wamuhifadhi mchezaji Gareth
Bale.
Spurs iliteleza kuingia katika michuano ya Klabu
Bingwa bara Ulaya katika michuano ya siku ya mwisho wa Ligi kuu ya
Uingereza baada ya Arsenal kuwafunga Newcastle 1-0 hivyo kumaliza ligi
wakiwa alama moja juu ya TottenhamKuna hofu kuwa mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda akahama kutokana na Spurs kushindwa kufunzi katika mashindano hayo ya bara Ulaya.
Lakini Villas-Boas amesema: "ikiwa tunataka kufaunye vizuri zaidi msimu ujao nilazima tushikilie hazina yetu na hilo ndilo nimekuwa nikifahamishwa tangu awali".
Bale, ambaye anadaiwa kunyemelewa na timu kadhaa maarufu miongoni mwao Real Madrid aliifungua Spurs bao lao la ushindi dhidi ya Sunderland siku ya mwisho wa Ligi kuu ya Uingereza.
Licha ya ushindi huo bado Spurs ilimaliza katika nafasi ya tano, ikiuwa nyuma ya Arsenal.
Villas-Boas amesisitiza kuwa msimu ujao timu yake itafufuka na kuwa katika nafasi bora zaidi ya kufuzu katika michuano ya Klabu bingwa bara ulaya.

No comments:
Post a Comment