
Bao dakika ya mwisho: David Luiz akifunga kwa mpira wa adhabu kuipa ushindi wa 2-1 Chelsea ugenini usiku huu

Shangwe zake: Luiz akishangilia baada ya kufunga

Penalti ya utata: Fabian Schar akiifungia Basle kwa penalti bao la kusawazisha
BAO la dakika ya mwisho la mpira wa
adhabu uliotinga moja kwa moja nyavuni la David Luiz limeipa ushindi wa
mabao 2-1 Chelsea katika Nusu Fainali ya kwanza ya Europa League ugenini
dhidi ya wenyeji Basle.
Awali, alinusurika kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kudaiwa kucheza rafu.
Refa Pavel Kralovec alitoa uamuzi wa
ajabu sana alipodai Luiz kamchezea rafu Cesar Azpilicueta kwenye eneo
wakati hakucheza na akawapa penalti wenyeji wakapata bao la kusawazisha
lililofungwa na Fabian Schar dakika ya 87.
Chelsea ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Victor Moses dakika ya 12.
Kikosi cha Basle kilikuwa: Sommer,
Philipp Degen, Schar, Dragovic, Park, Fabian Frei, Salah/Degan dk78,
El-Nenny/Zoua dk65, Die/Diaz dk61, Stocker na Streller.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Terry, Cole, Luiz, Hazard/Mata dk71, Ramires, Lampard/Oscar dk79, Moses na Torres.
Katika Nusu Fainali nyingine, Fenerbace imeilaza 1-0 nyumbani Benfica, bao pekee la Korkmaz dakika ya 72.
Katika Nusu Fainali nyingine, Fenerbace imeilaza 1-0 nyumbani Benfica, bao pekee la Korkmaz dakika ya 72.

Bao la kwanza: Victor Moses (kulia) akiifungia Chelsea


Sarakasi za shangwe: Winga Mnigeria akishangilia kwa sarakasi za aina yake

Malengo makubwa: Rafa Benitez anataka kuipa Chelsea taji la Europa League msimu huu

Mchawi: Hadi anatolewa, Eden Hazard alikuwa nyota wa mchezo
No comments:
Post a Comment