Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa
Arusha mjini na uvamizi onevu wa Polisi wakati huu wa usiku; Mh. Lema
amekubali kukamatwa na amechukuliwa na gari la polisi wakati huu na
kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha yaani Central Polisi.
Wananchi wengi wamejitokeza ku-support mbunge wao na huenda Asubuhi wananchi wakawa wengi zaidi.
Scene two ni hali itakavyokuwa huko polisi.
Updates
Sasa wamefika CLocktower anasindikizwa na msululu wa magari ya makada waliojitokeza ku-support kuelekea kituo cha polisi.
Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha amesachiwa na kuingizwa
ndani. Kamanda Lema alikuwa ameambatana na magari ya makamanda
waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.
Hivi sasa polisi wamewafukuza makamanda wote hapo kituoni na kuwaambia
hawatakiwi kuonekana hapo. Makamanda wameondoka kwa amani na kwenda
kupaki Safari hoteli wakisubiriana kupata mwongozo.
03:41am
Wamekutana pembeni ya kituo cha polisi na wamekubaliana kuwa watawanyike
wakalale hadi kesho asubuhi watajuzwa kinachoendelea. Hivyo, Lema yupo
ndani na wananchi waliomsindikiza wametawanyika kwenda kulala. Tutaonana
asubuhi kwa yale yatakayojiri.
SOURCE.JAMII FORUM
No comments:
Post a Comment