WEKUNDU
wa Msimbazi, Simba SC wamezinduka leo katika Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara na kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wao, kufuatia
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Uwanjwa Taifa, Dar
es Salaam.
Ushindi
huo, unaifanya Simba SC itimize pointi 34, baada ya kucheza mechi 19,
ikiendelea kubaki nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye pointi 37,
wakati wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wapo kileleni kwa pointi zao 45.
Hadi
mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyopatikana
ndani ya dakika tatu za muda wa nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 45
za kipindi hicho.
Coastal
ndio waliuanza vema mchezo huo, wakisukuma mashambulizi mfululizo
langoni mwa Simba na kama si uimara wa kipa Mganda, Abbel Dhaira
wangeweza kupata bao la mapema.
Ndani
ya dakika tatu, kipa huyo namba wa Uganda aliokoa michomo miwili ya
hatari, mmoja wa chini na mwingine wa juu na kuwafanya mashabiki wa
Simba warukwe kwa shangvwe, wakiamini wamepata kipa bora.
Ikumbukwe
hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa Dhaira kudaka katika Uwanja wa Taifa
tangu asajiliwe Simba SC dirisha dogo akitokea Iceland nay a pili katika
ardhi ya Tanzania, baada ya Simba na Bandari Kombe la Mapinduz
Zaidi
ya hapo, Dhaira alidaka dakika 45 kila mechi katika mechi mbili za
kirafiki nchini Oman na dakika zote 90, wakati Simba ikilala 4-0 mbele
ya Recreativo de Libolo nchini Angola wiki iliyopita.
Mrisho
Khalfan Ngassa alikuwa wa kwanza kuwainua vitini wana Simba dakika ya
kwanza ya muda wa nyongeza, baada ya kumchambua kipa Shaaban Kado,
akimalizia gonga safi zilizosababisha kizazaa langoni mwa Wagosi wa
Kaya.
Haruna
Athumani Chanongo alipigilia msumari wa pili kwenye ‘jeneza’ la Coastal
hii leo dakika ya tatu wa muda nyonegza akimalizia kazi nzuri ya
Ngassa, kufuatia shambulizi la kushitukiza.
Kipindi
cha pili, Coastal walikianza tena kwa kasi na kufanikiwa na kupata bao
la kufutia machozi dakika ya 49 na ushei, lililofungwa na kiungo Razack
Khalfan aliyeunganisha krosi ya Twaha Shekuwe.
Baada
ya hapo, timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu na hadi kipyenga
cha refa Martin Sanya kutoka Morogoro kinapulizwa kuhitimisha mchezo
huo, Wekundu wa Msimbazi waliibuka kidedea.
Simba
SC ilichelewa kuingia uwanjani hii leo na kukosa hata muda wa kupasha
misuli moto, kutokana na matatizo ya kufungiwa hotelini.
Katika
mchezo huo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud
‘Chollo’, Miraj Adam, Hassan Hatibu, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Amri
Kiemba, Rashid Ismail/Saim Kinje, Abdallah Seseme, Haruna Chanongo na
Mrisho Ngassa/Ramadhan Singano ‘Messi’.
Coastal
Union; Shaaban Kado, Hamad Hamisi, Abdi Banda, Mbwana Hamisi, Philip
Mugenzi, Razack Khalfan, Daniel Lyanga/Twaha Shekuwe, Mohamed Athumani,
Deangelis da Silva, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Joseph Mahundi/Castory
Mumbara
No comments:
Post a Comment