Hatimaye
ule utata kuhusiana na mahala pa kumzika msanii Juma Kilowoko 'Sajuki'
umepatiwa jibu baada ya baba yake kukubali kuwa azikwe jijini Dar es
Salaam.
Kutokana na uamuzi huo, sasa msanii huyo aliyekuwa nyota
na kipenzi cha wengi enzi za uhai wake atazikwa keshokutwa Ijumaa
(Januari 4) kwenye makaburi ya Kisutu.
Awali, baba wa msanii huyo
alitaka mwanawe akazikwe kwao mkoani Songea. Hata hivyo, baada ya
kuketi na kujadili kwa kina na familia yake, akaamua kutangaza kuwa
mwanawe huyo kipenzi atazikwa jijini Dar es Salaam ili kutoa nafasi kwa
rafiki zake wengi aliokuwa akishirikiana nao katika kazi zake za kila
siku za kisanii kupata nafasi ya kushiriki mazishi yake.
Mzee
Kilowoko ametoa msimamo huo mpya leo hoo hii, ikiwa ni muda mfupi tu
baada ya kutangaza awali kuwa mwanawe atakwenda kuzikwa Songea.
Sajuki
amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa
amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi na kupumua kwa msaada wa
mashine kabla ya kuaga dunia mishale ya saa 1:00 asubuhi.
No comments:
Post a Comment