SIKU
chache baada ya kamati ya utendaji ya klabu ya Simba kutangza kuzivunja
kamati zake ndogondogo, mwenmyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden
Rage ameanza kuteua wajumbe wa kamati mbalimbali am,bapo ameanza na ya
Usajili ambapo amemrejeshea madaraka yake mwenyekiti wa awali, Zacharia
Hanspoppe.
Rage
ambayea aliamua kuzivunja kamati hizo kutokana na kutokuwa na mchango
wowote katika timu hiyo ambayo iliishia kushika nafasi ya tatu katika
mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodaco, amesema kwamba ameamua
kumrejesha Hansopppe katika nafasi yake kutokana na kutoa mchango mkubwa
katika zoezi la usajili na hasa kutumia fedha zake katika kusajili.
Amesema
katika kamati hiyo, Rage atashirikiana na Azim Dewji, Mbunge wa Korogwe
Steven Ngonyani maarufu kama 'Prof. Maji Marefu', Muhsin Ruhwey, Sued
Nkwabi na wengineo atakaowatangaza baadaye.
Rage ameongeza kuwa hivi karibuni atatatangaza wajumbe wa kamati nyingine baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwateua.
Awali
kulikuwa na kamati za Ufundi iliyokuwa chini ya Ibrahim Masoud
'Maestro', Kamati ya Nidhamu iliyokuwa chini Jamal Rwambow, Kamati ya
Fedha iliyokuwa chini ya Geofrey Nyange 'Kaburu' na Kamati ya
Mashindabno iliyokuwa chini ya Joseph Itang'are 'Mzee Kinesi'
SOURCE;DINNA ISMAIL
No comments:
Post a Comment