Chelsea leo imeilaza Tottenham mabao 4-2 katika mechi ya ligi kuu ya Premier ya England.
Tottenham ilipata kipigo hicho mbele ya
mashabiki wake katika uwanja wao wa White Hart Lane, mechi ambayo
ilikuwa ya kwanza kwa kocha Andre Villas Boaz dhidi ya klabu yake ya
zamani.Villas-Boas alifutwa kazi na Chelsea, mwezi Machi mwaka uliopita baada ya kuliongoza kwa muda wa miezi tisa pekee.
Chelsea, ilicheza mechi ya leo bila naodha wake John Terry, ambaye ameanza kutumikia adhabu ya kutoshiriki katika mechi nne zijazo na Chelsea baada ya shirikisho la mchezo wa soka nchini England, FA, kumpata na hatia ya kutumia lugha ya ubaguzi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand.
Chelsea ndiyo ilikuwa kuwa ya kwanza kufunga wakati wa mechi hiyo lakini dakika Moja baada ya kipindi cha pili kuanza William Gallas aliizawazishia Tottenham na dakika chache baadaye Jermain Defoe akaongeza bao lingine la kuiweka Tottenham mbele kwa mabao mawili kwa bila.
Wachezaji wa Chelsea hawakufa moyo na walianza kufanya mashambulizi zaidi katika lango la wenyeji wao na nyota wao Juan Matta, alifunga mabao mawili katika kipindi cha dakika tatu na kuiweka tena Chelsea kileleni.
Mashambulizi ya Chelsea hayakuishia hapo mchezaji wa ziada wa Chelsea Daniel Sturridge naye akaifungia Chelsea bao lake la nne.
No comments:
Post a Comment