tuwasiliane

Thursday, September 20, 2012

SIMBA YAJIKITA KILELENI


Mabingwa wa Tanzania bara Simba SC leo hii wameendeleza makali yao waliyoanza nayo ligi kwa kuitandika timu ya wanajeshi wa JKT Ruvu kwa mabao mawili kwa sifuri.
Simba ambao walicheza mchezo kwa dakika nyingi baada ya mshambuliaji wao tegemeo Emmanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza cha mchezo, walipata mabao yao kutoka kwa kiungo Amri Kiemba aliyefunga bao la kwanza na Haruna Moshi Boban aliyepiga kidude cha pili.
Kufuatia matokeo hayo Simba inaendelea kukamata usukani mwa ligi kwa kukusanya pointi 6, magoli matano ya kufunga na wakiwa hawajuruhusu nyvu zao kuguswa. Simba walishinda mechi ya kwanza ya ligi kwa 3 - 0 dhidi ya African Lyon.
Kwa upande mwingine huko jijini Mwanza Azam FC wametoka sare ya kufungana 2-2 na Toto Africa, wakati Tanzania Prisons wametoka 1 - 1 na Coastal Union ya Tanga, Kagera Sugar wametoka sare tasa na JKT Oljoro, huku Ruvu Shooting wakiifunga Mgambo JKT 2-1.
WAKATI HUO HUO, MJINI MOROGORO Mabingwa wa Afrika mashariki na kati, klabu ya Yanga ya Dar es Salaam leo hii imekula kichapo mabao matatu kwa nunge kutoka kwa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro.

Katika mchezo huo ambao umekuwa na matokeo hasi kwa upande wa timu ya Jangwani ulianza kwa kwa timu kusomana lakini dakika ya 11 ya mchezo akaipatia timu yake ya Mtibwa bao la kuongoza, kabla ya Juma Javu kuongeza la pili katika dakika ya 45 ya mchezo katika kipindi cha kwanza na timu zikaenda mapumziko Mtibwa wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili Yanga wakafanya mabadiliko kwa kuwaingiza Saimon Msuva na Stephano Mwasika kuchukua nafasi za Frank Domayo na David Luhende lakini haikusadia chochote. Dakika ya 66 akatoka Mbuyu Twitte na kuingia Didier Kavumbangu lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwa upande wa watoto wa Manji.
Dakika ya 77 ya mchezo alikuwa yule yule Juma Javu akaenda kumtungua golikipa Ally Mustapha Barthez goli 3 na la mwisho katika mchezo huo. Dakika ya 90 Yanga wakapata penati lakini Hamis Kiiza akashindwa kufunga na mwamuzi akapuliz kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo.

No comments:

Post a Comment