Tuesday, September 18, 2012
Ngassa atamani ufungaji bora
MRISHO Ngassa 'Anko' amefurahia kuanza kwa ushindi mnono mechi ya Ligi Kuu Bara katika kikosi chake kipya cha Simba, lakini akatoa la moyoni kwa kusema amekabidhi miguu yake yote kwa Mungu ili amjalie awe mfungaji Bora.
Ngassa kwa mara ya kwanza ameichezea Simba kwenye mechi ya ufunguzi ya ligi dhidi ya African Lyon jijini Dar es Salaam akitokea Azam FC wakaifunga mabao 3-0 ambapo ushindi huo ulichangiwa na mchango wake mkubwa kwenye timu.
"Najisikia furaha katika kikosi changu hiki kipya baada ya kuanza kwa ushindi wa kishindo."
"Hii ni dalili njema kwetu kama tutaendelea na msimamo huu kucheza kwa kujituma ili tusipoteze mechi," alisema.
source; mwanaspoti gazeti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment