tuwasiliane

Tuesday, September 18, 2012

Kocha wa Yanga aanza visingizio


lisema hakufurahishwa na tukio la kusubiriwa kwa chakula cha wachezaji wakati wakiwa Mbeya, dhidi yao walipatiwa huduma hiyo saa moja baadaye na kitendo hicho hakikuendana na hadhi ya klabu hiyo.

Mbali na hayo ameuambia uongozi kwamba haiwezekani timu ikapata matokeo mazuri wakati maandalizi yake hayaendani na dhamira hiyo, huku akiongeza kuwa katika maisha yake.

Alisema yeye hajawahi kulala kwenye hoteli ya hadhi ya chini kwenye nchi zote 20 za Afrika alizotembelea, na tano alizowahi kufanya kazi kama waliyolala wakati wakiwa jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.

Saintfiet alisema hata hivyo kuwa, sare ya bila kufungana ambayo timu hiyo ilianza nayo kwenye msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania wa mwaka 2012/ 2013 dhidi ya wenyeji Prisons haijawakatisha tamaa na kusisitiza kwamba Yanga haina hofu ya kutotwaa ubingwa msimu huu.

Hayo yalisemwa na Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet amesema kwamba hakuridhishwa na mazingira ya hoteli ambayo timu hiyo ililala ikiwa Mbeya huku akisema kwamba kitendo cha wachezaji kulala wawili katika kila kitanda kimoja kilimkera na kwamba hatarajii kuona mambo ya aina hiyo yakijirudia.

"Didier (Kavumbagu) na Twite (Mbuyu) walilala kitanda kimoja kidogo cha ukubwa wa chini ya futi nne huku wakiwa wamebanana sana... unadhani hao wanaweza kuamka na kucheza vizuri? Kwakweli sijafurahishwa na hali hii. Ni aibu.

Mbona tulipokuwa Kigali (Rwanda) tulilala kwenye hoteli nzuri inayofanana na hadhi ya timu yetu," alilalamika kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Hata hivyo, Saintfiet alisisitiza kuwa huduma 'mbovu' walizopata sio sababu kubwa ya mwanzo wao usiovutia wa sare dhidi ya Prisons.

"Kipa wao alionyesha kiwango kizuri kwa kuokoa mashuti matatu ya Kiiza (Hamis) na moja la Msuva (Simon). Tulicheza vizuri lakini si katika kiwango chetu cha juu," alisema Saintfiet.

Naye Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa, aliliambia gazeti hili kwamba wamepokea malalamiko ya kocha huyo na kuahidi kutofikia tena katika hoteli ya kiwango cha chini.

Alisema walitarajia kukutana na kocha huyo ili kupanga maandalizi ya timu yao, na kumueleza uwezo wa klabu yao kwa sasa na bajeti waliyonayo.

No comments:

Post a Comment