Thursday, September 13, 2012
MOISE KATUMBI NA MIPANGO YA KUIFANYA TP MAZEMBE MOJA YA KLABU KUBWA DUNIANI
"Badilini maono yenu, achaneni na mawazo potofu na anzani kuisadia Africa kwa sababu Africa inajisaidia yenyewe."
Hizo ni kauli zinazotolewa na Jerome Champagne, mkurugenzi wa zamani wa mahusiano ya kimataifa katika chombo kinachoongoza soka duniani FIFA, ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mshauri wa timu ya TP Mazembe.
Raia huyu wa Ufaransa anaamini klabu hiyo ya Jamhuri ya Congo ipo kwenye mstari wa mbele wa mabadiliko, chini ya umiliki wa Moise Katumbi.
Mwaka 2010, Mazembe walitengeneza historia ya kuwa klabu ya kwanza ya Africa kuweza kufika fainali ya klabu bingwa ya dunia na Champagne anahisi mafanikio hayo ni ushahidi wa namna timu hiyo ilivyojipanga kupata mafanikio kwa klabu na bara zima kwa ujumla.
Aliiambia BBC Sport: "TP Mazembe ni taasisi itakayoiletea sifa kubwa Africa.
"Ni suala la kuueleza au kuuonyesha ulimwengu kwamba Africa haijalemaa - Africa inaendelea mbele ikiwa na viongozi wapya, watu sahihi kabisa walio na mapenzi na kazi zao, waaminifu, na wafanyakazi kwa bidii.
"Kitu ambacho Mr.Katumbi anajaribu kufanya na Mazembe ni kutuma ujumbe kwa ulimwengu: 'hey, ndio tuna matatizo huku lakini tuna mbinu nzuri na uwezo mzuri hivyo tutafanikiwa."
Mazembe ni washindi wa mara nne wa kombe la mabingwa wa Africa, kombe lao la hivi karibuni ni mwaka 2010, na sasa tayari wapo kwenye nusu fainali ya champions league ya msimu huu. Lakini bado klabu haijulikani sana nje ya Africa.
Mwanadiplomasia wa zamani Champagne ameletwa katika klabu hiyo na Katumbi kusaidia kuleta mbadiliko na kuhakikisha kwamba mafanikio ya uwanjani yanawiana na umaarufu wa klabu nje ya dimba.
Ana uhakika kwamba kwa uwezo wa kifedha wa na maono ya mfanayabishara tajiri Katumbi, klabu hiyo kutoka Lubumbashi inaweza kuwa moja ya timu kubwa sana katika ulimwengu wa soka.
"Mr Katumbi amefanya kazi nzuri sana katika kuifanya klabu kuwa washindi wa pili katika FIFA Club World Cup mwaka 2010. Na hataki hilo liwe la mwisho. Anataka mafanikio zaidi," aliendelea Champagne.
"Majukumu yangu ni kumsaidia kimataifa, kumsaidia katika mawasiliano na mambo ya kisiasa.
"Ana maono ya kuifanya klabu hii kuwa na nguvu na yenye kujitegemea zaidi. Anataka klabu kuwa na makubaliano na klabu nyingine barani ulaya na America ya kusini ili kuweza kufaidika kutokana na uzoefu kutoka kwenye hizo klabu.
"Mazembe inaweza kutuma wachezaji kwenye klabu hizo kwa ajili ya kujifunza na kupata uzoefu zaidi kwa staili tofauti. Lengo letu ni kuweza kushindana katika level ya dunia.
"Suala hili halitawezekana ndani ya usiku mmoja. Lakini kwa mfano tumeanza kwa kuweka lugha ya kiingereza kwenye mtandao wa TP Mazembe, ambao mwanzoni ulikuwa na lugha moja tu ya kifaransa.
"Tunaamini tuna vitu vingi sana ambavyo mashabiki wa TP Mazembe duniani kote wanapaswa kujua nini hasa Mazembe inafanya."
Wakati baadhi ya watu wanaweza wakahisi TP Mazembe wanafanikiwa kwa sababu tu ya utajiri wao wa mmiliki, Champgne anajaribu kuelezea maoni yake kwamba inachukua zaidi ya fedha nyingi kutengeneza klabu.
"Fedha sio kila kitu," anasisitiza. "Kitu kinacholeta utofauti hapa ni Mr Katumbi sio tu kwa sababu ana fedha za kuwekeza lakini ni mvumilivu.
"Inabidi uwasaidie watoto wakue, kutengeneza staili ya timu itakavyocheza na filosofia ya timu kwa ujumla inahakikisha wachezaji wanakuwa wanafanya mambo yao kwa adabu na kufuata kanuni na sheria mlizojiwekea - hivyo wanavyosafiri wawe ndio kioo na kinawachowakilisha klabu na heshima na maadili ya nchi waliyotoka
"Mr Katumbi na maono mazuri na mvumilivu. Na suala kupeana muda ni muhimu sana kwenye soka.
"Sio rahisi kwa sababu unaweza kufanya kazi vizuri kwa muda mrefu lakini unaweza ukapoteza kwa sekunde 10 kutokana na vitendo vya mchezaji vya ukosefu wa nidhamu - hivyo mambo yeote mazuri ya mwaka mzima yanaweza yakaharibiwa na kosa moja tu.
"Soka inaweza ikawa na ukatili mkubwa lakini huo ndio uzuri wa mchezo huu."
"Mchezo huu ni wa dunia nzima na sio mchezo wa kikundi cha watu fulani. Kila nchi ina haki ya kuendelea na kushiriki. Kila bara lazima lipokee nafasi sawa katika kushiriki na kushinda.
"Mipango ya Mazembe ni mizuri sana na ndio maana najisikia vizuri kufanya kazi hapa. Najisikia amani sana kuwa sehemu ya klabu, filosofia na kuweza kuwa karibu na Mr Katumbi ambaye anandoto ya kuifanya Mazembe kama ilivy Manchester United.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment