tuwasiliane

Saturday, September 1, 2012

01 SEPT.Lady Gaga amshika pabaya Lindsay


WAKATI suala la wizi wa vito vya thamani linalomkabili, Lindsay Lohan likiwa halijatulia, Lady Gaga amechafua hali ya hewa kwa kuibua mjadala mtandaoni.

Lady Gaga aliposti picha ya Lindsay katika mtandao wa twitter na kuuliza hereni alizovaa hajaiba nyumbani kwake kwani hivi sasa haaminiki.

Inawezekana Gaga alifanya hivyo kwa kumtania mwanamuziki huyo lakini mashabiki wake walianza kubeza kwa kuandika maneno ambayo yalimdhalilisha Lindsay.

Saa mbili baadaye, Gaga baada ya kuzidiwa na maneno ya kejeli dhidi ya Lindsay aliamua kuitoa picha hiyo lakini mashabiki waliendeleza mjadala.

Baadaye Lindsay naye aliandika katika mtandao wake kwa kifupi: "Sijakasirishwa na kitendo hicho ila nashukuru kwa yote yaliyotokea

No comments:

Post a Comment