Thursday, August 30, 2012
30 AUG.Keita apewa miaka miwili Simba
MWENYEKITI wa Kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope amesema kuwa wameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na mchezaji, Komabil Keita na tayari wameingia naye mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.
Hans pope alisema kuwa hivi sasa wanamalizia mazungumzo na klabu aliyotoka na wapo katika hatua ya mwisho ili wamuombee hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC).
Alisema kuwa wameamua kumsajili mchezaji huyo baada ya mchezaji wao Mussa Mudde kuumia mguu na kutakiwa kukaa nje kwa muda huku akipatiwa matibabu.
Hans Pope alisema wataendelea kukaa na Mudde huku wakimtibu mpaka atakavyopona na hawatakatisha mkataba na mchezaji huyo kama ilivyoripotiwa awali.
Hata hivyo, Mudde alipoulizwa na CHANZO CHETU kuhusu suala hilo alisema hakubaliani na jambo lolote la kukatwa au kutolewa kwa mkopo kwenda timu yoyote.
Mudde alisema kwa njia ya simu kuwa yeye hafahamu maendeleo mengine kuhusiana na usajili wake na Simba zaidi ya kusubiri apone na kuja kuitumikia klabu hiyo tofauti na taarifa kuwa amekubaliana na uongozi wa klabu hiyo kuhusiana na kutoichezea timu hiyo kutokana na kuwa majeruhi.
Alisema kuwa yeye anasoma habari zake kupitia mitandao na kushangazwa na taarifa hizo kwani sio za kweli.
ìMimi nilikuwa Tanzania (Dar es Salaam) hivi karibuni, niliitwa na uongozi, lakini mbali ya kuzungumza masuala ya matitabu, hatujazungumza suala lingine kuhusiana na mabadiliko ya mkataba, kuvunja, kutolewa kwa mkopo au utaratibu mwingine, baada ya kumaliza mazungumzo hayo nilirejea nyumbani, kwa kifupi sikubaliani na suala lolote kinyume na mkataba wangu,î alisema Mudde.
Alisema kuwa viongozi wa Simba wanatakiwa kuongea mezani tofauti na taarifa za sasa ambazo yeye anazipta kwa njia ya vyombo vya habari au kupigiwa simu na watu wake wa karibu.
ìLengo langu ni kucheza mpira na nimeumia nikiwa ndani ya Simba, nashukuru kwa kunitibia na sasa naendelea vizuri, ila mipango yao ya sasa ambayo itanifanya nikae nje ya klabu, si kubaliani nayo,î alisema.
Alisema kuwa anaamini kuwa viongozi wa Simba watafuata taratibu kwa mujibu wa sheria na kuiomba Shirikisho la Kandanda nchini (TFF) kuwa makini na suala hilo na wasikubaliane na jambo lolote mpaka kuwe na makubaliano.
Kigingi hicho cha Mudde kinalifanya suala hilo kuwa gumu kwa Simba na hiyo inatokana na taarifa za Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura kuwa makubaliano baina ya oande hizo mbili ndiyo kigezo cha wao kupitisha maamuzi.
Simba kwa sasa ina wachezaji sita wa kigeni kinyume na taratibu za TFF ambazo zinawataka kuwa na wachezaji watano. Wachezaji hao ni Paschal Ochieng (Kenya), Emmanuel Okwi (Uganda), Felix Sunzu (Zambia), Mudde (Uganda) na Daniel Akuffor wa Ghana.
Wambura alisema kuwa endapo Simba watakubaliana na mchezaji huyo kama ilivyokuwa kwa Danny Mrwanda wanaweza kufanikisha malengo yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment