tuwasiliane

Wednesday, August 29, 2012

29 AUG.Mudde apigwa panga Simba



KOCHA wa Simba, Milovan Cirkovic ameondoa utata wa wachezaji wa kigeni ndani ya Simba baada ya kutamka kwamba atamchomoa kiungo Mussa Mudde kikosini kutokana na majeruhi yanayomkabili.

Mudde aliyetamba Simba kwenye michuano ya Kagame akitokea Sofapaka ya Kenya, anakabiliwa na tatizo la kifundo cha mguu ambacho hakijapata nafuu.

Kwa mujibu wa Milovan, mchezaji huyo hatakuwa uwanjani kwa mzunguko mzima wa kwanza jambo ambalo litaigharimu Simba kama itamvumilia.

Mudde kuna uwezekano mkubwa nikamtoa kikosini wakabaki hao wengine watano kwa kuwa majeruhi yake ni ya muda mrefu sana, alisema.

Hawezi kupona ndani ya mwezi mmoja na hata kama akipona lazima atumie muda kuwa fiti, hata kupata namba kwenye kikosi cha kwanza kwa kuwa kiungo kina wachezaji wengi na kila mmoja yuko fiti.

Ni mchezaji mzuri lakini hakuna jinsi anaweza kuhimili ushindani uliopo kutokana na majeruhi yake, nitatoa nafasi kwa hawa wachezaji ambao wako fiti kwa sasa kwa kuwa tunaingia kwenye ligi ngumu na tunatakiwa kuwa na timu nzuri zaidi yenye wachezaji ambao ni tayari kutumika muda wowote,alisisitiza.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange alisema watatoa tamko rasmi wiki hii kuhusiana na mchezaji huyo ingawa Mwanaspoti linajua Milovan amebariki aachwe.

Wachezaji wa kigeni watakaobaki Simba ni Emmanuel Okwi(Uganda), Paschal Ochieng(Kenya), Komabil Keita(Mali), Daniel Akufor (Ghana) na Mzambia Felix Sunzu.

Mastaa wapya wa kigeni kutoka Mali, Ghana na Kenya wamemvutia kocha hususani Akufor na kocha amekuwa akiwasifia waziwazi mazoezini.

SOURCE; MWANASPOTI

No comments:

Post a Comment