tuwasiliane

Wednesday, August 29, 2012

29 AUG.Arsenal kukongoroka;Walcot nae kuondoka


Habari za kuaminika zasema kuwa klabu ya Arsenal inatathmini kumuuza mshambuliaji wake Theo Walcott kabla ya dirisha la usajili kufungwa mnamo siku ya Ijumaa.

Mchezaji huyo mwenye sifa ya kasi kwenye upande wa kulia wa uwanja ana mda wa mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Arsenal.

Tangu aondoke aliyekuwa nahodha msimu uliopita, Robbin Van Persie, Walcot aliyesajiliwa kutoka klabu ya Southampton kwa kitita cha pauni milioni 9.1anaonekana kuwa aliyetetereshwa na kuondoka kwa nahodha huyo.

Habari hizi huenda zitawasumbua mashabiki wa klabu hio ya London ya kaskazini ingawa hadithi hii imeviamsha vilabu kama Liverpool na Man.City vinavyommezea mate na Arsenal itatazamia kutengeneza senti zaidi.

Shirika moja la habari za michezo limearifu kuwa Walcot amekataa mpango wa klabu hiyo wa pauni milioni 4 kwa kila mwaka na huenda akauzwa kabla ya kufungwa kwa dirisha siku ya Ijumaa.

Inaaminika kuwa Wacot anataka alipwe pauni 75,000 kwa kila wiki, katika mkataba mpya badala ya kuu wa sasa unaomalizika mwakani.

Inaaminika kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 alitaka malipo yake yapandishwe hadi pauni £100,000-kwa kila wiki au karibu na hizo na ikiwa atashindwa kuafikiana na Arsenal katika mda wa saa 48 huenda ukawa mwisho wa miaka yake sita na nusu akiichezea Arsenal.

No comments:

Post a Comment