tuwasiliane

Monday, August 13, 2012

13 AUG. WABUNGE WATAKA BUNGE LISIONESHWE LIVE


Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema baadhi ya wabunge wanataka vikao vya Bunge, visiwe vinaonyeshwa moja kwa moja kwenye television.

Pamoja na maoni hayo, amesema suala hilo linahitaji mjadala mkubwa kwa kuwa kitendo cha kutoonyesha vikao vya Bunge, ni sawa na kurudi nyuma tulikotoka, badala ya kuendelea mbele.

“Kuna baadhi ya wabunge wanataka Bunge lisiwe linaonyeshwa ‘live’, wao wanataka Bunge lionyeshwe ‘live’, wakati wa kipindi cha maswali na majibu na baada ya hapo ‘tu switch off’ hadi jioni, wakati wa kupitisha vifungu.

“Hili jambo siyo jambo rahisi, kwa sababu kitendo cha kuanza kuonyesha ‘live’, Bunge letu maana yake tumesonga mbele, sasa tukitaka ‘ku switch off’ maana yake tunarudi nyuma.

“Tena hili jambo lina ‘movement’ kubwa na wanasema wakati Bunge lilipokuwa halirushwi ‘live’, baadhi ya wabunge walikuwa hawafanyi wanayoyafanya na kwamba wanayoyafanya sasa ni kwa sababu wanataka waonekane kwenye television.

“Wanajenga hoja nyingine kwamba, television za nini wakati magazeti yapo? yaani television zionyeshe halafu kesho asubuhi ninunue magazeti, wanasema haiwezekani.

“Lakini yote kwa yote, jambo hili linahitaji mjadala kidogo maana hatuwezi kurudi tena nyuma,” alisema Naibu Spika kwa kifupi.

No comments:

Post a Comment