tuwasiliane

Wednesday, July 18, 2012

18 JUL. OFFICIAL; IBRAHIMOVIC ATUA PSG



KLABU ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa, imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa Zlatan Ibrahimovic (pichani) kutoka AC Milan ya Italia. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Sweden, amesaini mkataba wa miaka mitatu, ambao utamuweka Parc des Princes hadi mwaka 2015, huku klabu hiyo ya Mji Mkuu wa Ufaransa, ikiripotiwa kutumia kiasi cha Euro Milioni 23 kuinasa saini ya mpachika mabao huyo wa zamani wa Inter Milan ya Italia pia na Barcelona ya Hispania.

No comments:

Post a Comment