tuwasiliane

Wednesday, July 18, 2012

18 JUL. BREAKING NEWZ; MELI YA SEAGUL YAZAMA





Taarifa zilizotufikia ni kwamba Meli ya Seagul iliyokuwa ikielekea visiwani Zanzibar ikitoka Dar es Salaam imezama muda huu. Meli hiyo ilitoka Dar es Salaam leo saa 7 mchana ikiwa na abiria karibia 200 na kuzama katika eneo la Chumbe jirani na Zanzibar. Mpaka sasa haijafahamika madhara yaliyotokana na ajali hiyo.

UPDATES

taarifa ambazo tumezipata hivi punde,kuwa maiti zaidi ya 12 zimepatikana na watu zaidi ya 120 wameokolewa.
pia tumepata taarifa kuwa katika boti hiyo kulikuwa na watu zaidi ya 281, na mizigo mingi sana hali iliyopelekea boti hiyo kwenda upande upande
UPDATES ZA MUDA HUU
Taarifa ya Serikali - Kuzama kwa Meli Zanzibar

MAAFA YA KUZAMA KWA MELI ZANZIBAR


Meli ya Mv. Star Gate imezama karibu na Kisiwa cha Chumbe ambapo watu 12 wamefariki hadi muda huu na wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Akitoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini alisema taarifa za kuzama kwa meli hiyo ilitolewa na Boti iendayo kasi ya Kilimanjaro III iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar ndipo ilipoiona meli hiyo ikizama.

“Tulipata taarifa kutoka Boti ya abiria ya Kilimanjaro III saa 7:50 mchana waliporipoti kuona meli ikizama karibu na Kisiwa cha Chumbe” Alisema Waziri Mwinyihaji.

Waziri huyo alisema Meli hiyo imezama maili sita kuelekea Kisiwa cha Yasin Kusini mwa Kisiwa cha Chumbe kilichopo Unguja maili kadhaa kutoka Bandari ya Malindi.

Waziri Mwinyihaji alisema idadi ya abiria walikuwa 250 ambao ni watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6. “Tumepeleka waokoaji, kuna boti tano zipo eneo la tukio kushirikiana na waokoaji wengine” Alisema Waziri Mwinyihaji.

Alisema maiti zote zitapelekwa viwanja vya Maisara Zanzibar kwa ajili ya ndugu na jamaa kuzitambua maiti za ndugu zao ambapo majeruhiwa wote watatibiwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.

Katika Bandari ya Malindi mwandishi wetu ameshuhudia maiti kadhaa zikiwemo za watoto zikishushwa, Miongoni mwa abiria waliookolewa ni raia 13 wa Mataifa mbalimbali ya nje huku raia mmoja ambaye hakuweza kutambuliwa utaifa wake amepoteza maisha.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd alifika eneo la Bandari ya Malindi Zanzibar pamoja viongozi wengine akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Mawaziri na baadhi ya Wajumbe a Baraza la Wawakilishi walikuwepo kutoa msaada unaohitajika.

Katika eneo la pembezoni mwa bandari ya Malindi, makundi ya wananchi yalikuwa yamekusanyika wakisubiri taarifa za tukio hilo tangu saa 8:30 mchana.

Vikosi vya ulinzi na usalama, msalaba mwekundu na watoaji wengine wa misaada ya dharura walifika kwa haraka eneo la tukio.

Hadi sasa kazi ya uokoaji inaendelea karibu na Kisiwa cha Yasin ilikozama meli hiyo.

Meli ya Mv. Star Gate inamilikiwa na kampuni ya kizalendo ya Sea Gull Sea Transport Ltd ambayo mwaka 2009 Meli yake nyengine ya Mv. Fatih ilipinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi Zanzibar na kua watu sita.

Mwaka jana Zanzibar ilikumbwa na maafa baada ya Meli ya Mv. Spice Islanders kuzama katika bahari ya Hindi eneo la Nungwi katika Kisiwa cha Unguja ikielekea Kisiwani Pemba ambapo taarifa rasmi ya Serikali ilisema watu 197 walipoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.

Taarifa zaidi zitatolewa hapo baadea.

Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzíbar
Julia 18,2012


Zanzíbar,Tanzania

UPDATES
HABARI TULIZOZIPATA NI KWAMBA HADI JANA USIKU WAKATI WANASITISHA SHUGHUL ZA UOKOAJI MAITI 6O ZILIKUWA ZIMPATIKANA. ILIBIDI WASITISHE ZOZI LA UOKOAJI JANA USIKU KWA KUWA KULIKUWA NA HALI MBAYA SANA YA HEWA.

MASHUHUDA WALIOENDA SEHEMU YA TUKIO WANASEMA KUWA MELI ILIKUWA IMEPINDUKA KABISA KWA HIYO KUWEZA KUWAPATA WATU WENGINE WA KIWA HAI NI MAJALIWA YA MWENYEZI MUNGU.

HADI JANA JIONI HALI ILIKUWA TETE JIJINI DAR ES SALAAM, KWANI WATU WALIKUWA WAKIULIZIA TAARIFA ZA NDUGU ZAO LAKINI HAWAKUWEZA KUIPATA OFISI ZA SEAGUL, HALI ILIYOPELEKEA WATU KUJIULIZA MASWALI KWANINI KAMPUNI KUBWA KAMA HIYO ILIKUWA INAFANYA KAZI KIENYEJI, MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ZILIKUWA WAPI MUDA WOTE HUO.

Mtandao wako utazidi kukupa habari zaidi kuhusiana na tukio hili

No comments:

Post a Comment