tuwasiliane

Saturday, July 14, 2012

14 JUL. YANGA 0 ATHLETICO 2


Mabingwa wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Yanga leo wameduwazwa na mabingwa wa Burundi Atletico baada ya kuchezeshwa soka safi na nyavu zao kuguswa mara mbili, katika mchezo huo wa michuano ya kombe la Kagame linalo shikiliwa na yanga.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa taifa leo jioni, Yanga waliuwanza vyema mchezo kabla ya kuanza kuutafuta mpira toka miguuni mwa wa Burundi walio kuwa wakicheza kitimu zaidi. Yanga walionekana kupoteana na kila mchezaji kucheza kivyake na kukosekana umoja wa kitimu (team work).

Kazi nzuri iliyo fanywa nakipa wa yanga toka Ghana Yarw Berko ilipunguza idadi ya magoli kwa Atletico na kupelekea yanga kufungwa goli 2-0, badala ya 6 kama asingetumia uwezo binafsi kuzima mashambulizi ya Atletico.

Iliwachukuwa dakika 82 kwa Waburundi hao kuandika goli la kwanza kupitia kwa Didier Kavumbagu, ambaye alirejea tena nyavu katika dakika za lala salama, hivyo kuitoa kifua mbele Atletico katika mchezo huo.

Baada ya kichapo hicho katika mchezo wa kwanza wa Kagame kocha wa Yanga, Saintfiet amekubali mziki wa Atletico huku akitupia lawama wachezaji wake katika mchezo huo ambao yanga ilijazwa na wachezaji wageni katika timu hiyo.

"Hata nilipowaambia wabadilike, wachezaji waliamua kuendelea kucheza mpira wa pasi fupi fupi badala ya kucheza wa moja kwa moja wa kwenda mbele. Hauwezi kushinda hata siku moja kama utacheza bila kumsikiliza kocha. Kulikuwa na udhaifu katika eneo la ulinzi wa kati."

"Hakuna visingizio, wenzetu wamecheza vizuri sana. Ni mabingwa wa nyumbani kwao Burundi na walicheza mechi ya kujiandaa dhidi ya timu ya Congo na wakashinda 4-1 na tulifahamu hilo kabla. Nawapongeza ni timu nzuri sana, walikuwa ni matawi ya juu dhidi yetu leo," alisema Saintfiet


Katika mchezo wa awali wa Kundi A ambalo ndio kundi la Yanga,APR ya Rwanda wameibuka na ushindi mnono wa goli 7-0 mbele ya wageni toka South Sudan Wau Salaam.

Kwa matokeo yam mchezo hiyo ya leo ya kundi A. Kundi hilo kwa sasa linaongozwa na APR, ikifuatiwa na Atletico wote wenye point 3. APR akiwa na faida ya goli 7 wakati Atletico wakiwa na 2.

Yanga inashika nafasi ya taut wakiwa hawana point sawa na Wau Salaam waliofunwa magoli 7 wakati Yanga wakifungwa 2. Timu 3 za juu toka kundi hili litatinga hatua ya Robo fainali.


Michuano hiyo itaendelea kesho kwa michezo mitatu ya Kundi B na C, ambapo Simba SC watakuwa uwanja wa Taifa saa 10 jioni kuwakabili URA wakati huo Azam FC wakiwa Chamanzi kuwakabili Mafunzo. Mchezo wa awali utachezwa katika uwanja wa Chamanzi utakuwa kati ya Vital O ya DRC dhidi ya Ports.

No comments:

Post a Comment