
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema kwamba klabu yake imewaacha wachezaji hao, na kati yao kuna waliomaliza mikataba yao huku wengine kupelekwa kwa mikopo klabu nyingine za Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mchakato wa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara kuwasilisha majina ya wachezaji wanaoachwa ama kumaliza mikataba unafikia tamati kesho.
Si wengine bali ni wale Mabingwa wa mpira wa soka Afrika Mashariki na kati, Yanga ya hapa Jijini wametangaza kuwatema wachezaji wake 11 kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Wachezaji walioachwa ni pamoja washambuliaji wa kimataifa, Mghana Keneth Asamoah na Mzambia Davies Mwape, huku wengine wakiwa Iddi Mbaga, Julius Mrope, Kiggi Makassi, Atif Amour, Abuu Ubwa, Zuberi Ubwa, Bakari Mbegu, Godfrey Bonny na Shaban Kado ambaye amepelekwa kwa mkopo Mtibwa Sugar.
Sendeu alisema kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi yake, ambapo kesho kitashuka ndani ya dimba la taifa hapa Jijini kumenyana na mechi ya kimataifa ya kirafiki na mabingwa wa soka nchini Uganda, Express.
Kwani Express ilitarajiwa kuwasili hapa Jijini jana, ambapo kiingilio kitakuwa ni sh 20,000 kwa VIP A, sh 15,000 VIP B na C, sh 5,000 kwa watakaokaa viti vya kijani na wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na chungwa watalipa sh 3,000.
Mbali na hilo klabu hiyo leo inatarajiwa kuendesha kisomo maalum ‘hitma’ kwa ajili ya kuwarehemu wanachama, mashabiki, wapenzi na wachezaji wa timu hiyo waliotangulia mbele ya haki, ambapo zoezi hilo litafanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko mitaa ya Jangwani na Twiga na kuongozwa na Katibu wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali.
No comments:
Post a Comment