
Hatimaye klabu ya Orlando Pirates imetuma rasmi barua ya mualiko kwa mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kufanya majaribio ya kuweza kujiunga na timu hiyo.
Nimefanikiwa kuiona barua hiyo,COPY YAKE IPO HAPO JUU ikiwa inatoa maelekezo kwamba Okwi atapewa majaribio ya wiki mbili na Orlando Pirates, huku akihudumiwa kuanzia usafiri, malazi, matibabu pamoja na gharama nyingine zitakazojitokeza kwa wakati atakaokuwa na klabu hiyo.
Kwa kipindi cha misimu miwili sasa Orlando wamekuwa wakimfuatilia Okwi ambaye klabu yake ya Simba imemuwekea price tag ya Billioni 2 kwa timu inayomtaka, huku pia wapinzani wao wa jadi klabu ya Yanga ikiwa inamfukuzia mshambuliaji huyo wa Uganda ambaye siku za hivi karibuni amekuwa ndio tegemeo la safu ya ushambuliaji ya mabingwa wa Tanzania.
SOURCE; SHAFFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment