tuwasiliane

Wednesday, May 30, 2012

30 MAY; OFICIAL, SHIBOLI ATUA POLISI MOROGORO


MSHAMBULIAJI wa zamani wa Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara , Simba ya jijini Dar es Salaam, Ally Ahmed Ally ‘ Shiboli’ amesaini mkataba wa mwaka kuichezea timu ya Polisi Morogoro.

‘Shiboli’ ambaye amewahi kuichezea timu ya KMKM ya Zanzibar, kabla ya kujiunga na Wekundu wa Msimbazi Simba na baadaye kwenda Coastal Union, amesaini mkataba huo jana mjini hapa mbele ya viongozi Polisi.

Akizungumza na Chanzo chetu baada ya kusaini mkabata huo Shiboli alisema amejiunga kwa mapenzi yake na kwamba ataitumikia timu hiyo kwa juhudi zake zote.

“Nimechezea timu mbalimbali KMKM, Simba, Coastal Union na sasa nipo Polisi Morogoro …nitaisaidia kwa juhudi zagu zote kwa vile sasa mimi ni mchezaji wa Polisi” alisema.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Polisi Clamence Banzo, alisema kuwa uongozi wa timu umefurahi kupata mchezaji huyo ambaye ataisaidia timu hiyo katika Ligi Kuu inayotarajiwa
kuanza Agosti.

“Nashukuru kupata saini yake Ally Shiboli …lengo letu ni kusajili wachezaji kulingana na mapendekezo ya Kocha Mkuu wetu John Simkoko, nia ni kutaka kuijenga timu iwe ya mfano na irudishe heshima ya Morogoro na kujenga matumaini ya kila mtu kwa timu yao,”
alisema Banzo.

No comments:

Post a Comment