
CHAMA cha Soka cha Malawi (FAM), kimeomba mechi ya kirafiki ya kimataifa baina ya timu yao ya taifa na Taifa Stars ambapo kimependekeza ipigwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kati ya Mei 24 na 28 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
juzi, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Angetile Osiah ‘Ngeta’, alisema kuwa Malawi pia imeomba kucheza mechi nyingine zaidi na timu yoyote na TFF imeipendekeza Simba.
Alisema kuwa TFF imeamua kuipa Simba nafasi hiyo, kwa kuwa ina nafasi kubwa ya kusonga mbele katika hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, (CAF), hivyo mechi hiyo itaisaidia katika maandalizi ya hatua inayofuata.
Aliweka wazi kuwa pamoja na kuipa nafasi hiyo Simba lakini bado hajawasiliana na viongozi wa klabu hiyo kutokana na matatizo ya mawasiliano lakini matarajio yao ni kuwa watairidhia mechi hiyo kwa kuwa itawasaidia wao pia.
“Kwa sasa mazungumzo baina ya mkurugenzi wao wa ufundi Jack Chamangwana na mkurugenzi wetu wa ufundi Sunday Kayuni yanaendelea na yakikamilika tutawatangazia mechi hizo zitachezwa lini,” alisema Ngeta.
No comments:
Post a Comment