
Taarifa ya habari iliyosomwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) saa saba mchana wa leo inasema kuwa Mahakama imetengua Ubunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa.
Matokeo hayo yametenguliwa katika kesi ya pingamizi la ushindi wa Mbunge huyo iliyofunguliwa na mgombea wa CHADEMA kufuatia kasoro zilizojitokeza wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 na kwamba kiti hicho kilichokuwa kikishikiliwa na Aeshi Khalfan Hilaly, CCM, sasa kipo wazi.
No comments:
Post a Comment