tuwasiliane

Tuesday, April 24, 2012

24 APR.PHD akanusha kuzusha kifo cha Sajuki!


Siku nzima ya jana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kulizuka taarifa au tetesi ya kifo cha muigiza na director wa movie za kibongo maarufu kwa jina la SAJUKI.



Kutokana na taarifa hiyo lawama zote zikamuangukia Actor ambaye pia ni mwimbaji wa Bongo Flava artist mtu mzima Hemedy PHD ambaye inadaiwa ndiye aliyeandika taarifa hizo kwa mara ya kwanza katika status yake ya facebook kuwa eti SAJUK ameaga dunia.



Lakini baada ya kuulizwa kwa njia ya sms Hemedy alikanusha kuwa yeye hausiki kabisa nakuandika taarifa hizo ila kuna njemba imefungua page ya facebook kwa jina lake Hemedy PHD na kusambaza uzushi huo.

No comments:

Post a Comment