tuwasiliane

Tuesday, April 24, 2012

24 APR.Amnywesha sumu DOGO, kisa 15,000!

Katika hali ya kuogofya mwanadada mmoja wa Manispaa ya Lindi, aliyefahamika kwa jina la Lucy Cassian, anatuhumiwa kumpa mtoto wake wa kumzaa Richard Said (miezi minane) dawa ya kusafishia vidonda kwa kumnywesha ili afe kwa nia ya kupewa Sh 15,000 na mumewe ili afanyie biashara. Akielezea ukatili alioufanya Mama wa mtoto huyo alisema alimwomba fedha mumewe, Said Richard, lakini badala yake, mume huyo anadaiwa kumshawishi amuue mtoto huyo ili amkopeshe 15,000 kwa nia ya kumsaidia kufanyia biashara. Alidai mumewe huyo alishawahi kusema kuwa huyo mtoto siyo wa kwake. Kwa mujibu wa mdada huyo hapo awali alipewa na mumewe Sh 1,000 ambazo Sh 500 anunue sabuni na Sh 500 atumie kwa kunywa chai na kuamua kuondoka kwenda kwa mwanamke mwingine aliyezaa naye anayeishi Mnazi Mmoja. Alisema ilipofika saa nane mchana, aliamua kuitoa dawa hiyo na kumnywesha mtoto, na haikuchukua muda, alifika mwanamke aliyemtaja kwa jina la Mama Shabani na kumwokoa kwa kumtafutia maziwa yaliyochanganywa na chumvi na hatimaye alipona na kumkimbiza hospitalini.

No comments:

Post a Comment