tuwasiliane

Monday, April 23, 2012

23 APR. SIMBA YAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA




Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa kwa ngazi klabu, Simba SC wameendelea kuusogelea Ubingwa wa Tanzania Bara baada ya Kuwachapa Moro united goli 3-0, huku mchezo wawapinzani wake katika mbio za ubingwa Azam FC ukivunjika matokeo yakiwa sare ya goli 1-1.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom Simba SC waliandika goli la kwanza kupitia kwa Patrick Mafisango, huku Haruna Moshi Boban akiiandikia goli la pili Simba.

Simba walihitimisha goli la 3 kupitia kwa Felixs Sunzu, na mpaka kipenga cha mwisho Simba SC 3-0 Moro united.

Kwa matokeo hayo Moro United waungana na Polisi Dodoma katika kushuka daraja, na kuziacha Villa Squad na African Lyon zikichuana kujinusuru kushuka daraja.

Timu tatu za mwisho ndizo zitakazo shuka daraja na nafasi zao kuchukuliwa na Prisons ya Mbeya, Polisi Morogoro na JKT Mgambo Shooting ya Tanga katika msimu ujao.


Katika mchezo mwingine uliochezwa Chamanzi kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar ulivunjika baada ya Mtibwa Sugar walio kuwa pungufu kugomea penati ya Azam FC katika dakika za majeruhi.

Mchezo huo ulivunjika matokeo ya kiwa goli 1-1. Magoli yakiwa yamefungwa na Salum Swedi kwa upande wa Mtibwa na Mrisho Ngassa kwa upande wa Azam FC.

Kutokana na Sheria za Ligi kuu Azam FC wamepewa ushindi wa goli 2-0 kutokana na Mtibwa Sugar kupelekea mchezo kuvunjika kwa kutoka uwanjani baada ya Azam kupewa penati hiyo, inayodaiwa haikuwa halali.

No comments:

Post a Comment