tuwasiliane

Friday, April 20, 2012

20 APR.BREAKING NEWS……..mawaziri Mkulo, Chami, Nyundu na Mponda waachia ngazi


Habari mvunjiko ambazo zimetufikia Jukwaa Huru ni kwamba, mawaziri wanne katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameamua kuachia ngazi baada ya wajumbe wa kamati ya uongozi ya CCM kukutana kwa dharura mjini Dodoma jioni ya leo.

Mwandishi wa habari wa Jukwaa Huru ambaye amekuwa akifuatilia taarifa hizi, amejaribu kuwasiliana na mmoja wa wajumbe walioshiriki kikao hicho ambapo licha ya kushindwa kupokea simu, chanzo hicho cha habari kimeweza kuthibitisha uwepo wa tukio hilo baada ya kumjibu mwandishi wetu kwa ujumbe mfupi akisema “kama unachotaka kujua ni hicho, ni kweli”

Taarifa za awali zinaeleza kuwa waliojiuzulu ni pamoja na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo, Naibu waziri wa Afya Haji Mponda, Waziri wa Uchukuzi Bw, Omari Nundu pamoja na Dk. Cyril Chami

Taarifa zaidi zitakujia baadae

SOURCE www.jukwaahuru.com

1 comment:

  1. waachie na cc vijana 2chukue nafac zao maana wamezeeka na bado wanataka wale tu. wacpewe madaraka yoyote ktk nchi hii wezi wakubwa hao.

    ReplyDelete