Friday, April 13, 2012
13 APR. MBOWE;Hatuwezi jenga ofisi kwa 'WALIOLALA'
Chairman wa Chadema, Freeman Mbowe amekataa ombi la kupeleka makao makuu ya chama hicho mkoani Dodoma.
Ombi hilo lilitolewa juzi kwenye mkutano wa hadhara na Diwani wa chama hicho wa Kata ya Makulu mkoani Dodoma, Ally Biringi.
Akikataa ombi hilo Mbowe alisema “Kwenye maeneo ambayo chama kimejengeka, ujue wenyeji wameamka, wamejitoa mhanga na hata kuuawa… hapa Dodoma bado mmelala, huwezi kuhitaji mabadiliko mkaogopa polisi halafu mnategemea Kamanda Mbowe awajengee ofisi, hilo haliwezekani,” alisema Mbowe.
Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema Dodoma wanachelewesha wananchi wenzao kwa kushindwa kuleta mabadiliko kutokana na wabunge wote wa Mkoa wa Dodoma kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Dodoma wamelala…wenyeji wenyewe wanasinzia hawataki kujenga chama na Mbunge mashuhuri wa misamiati ya matusi anatoka mkoani Dodoma,” alisema Mwenyekiti huyo. Hata hivyo hakumtaja mbunge huyo. ila anajulikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment