Thursday, April 5, 2012
05 APR.Setif yatishia kugoma
Habari kutoka Algeria zinasema, nahodha wa timu hiyo Mourad Delhoum aliyezungumza kwa niaba ya wenzake alisema taarifa hizo wameziwasilisha kwa uongozi wa klabu hiyo Juu ya kulipwa mishahara yao ya mwezi uliopita.
Madai makubwa ya wachezaji hao mishahara yao pamoja na posho za ligi ya ndani na michuano ya kimataifa ambapo walikumbusha kuwa waliwaonya viongozi wao walipokuwa
Dar es Salaam kucheza na Simba wiki mbili zilizopita kwamba wanataka walipwe fedha zao.Wachezaji hao wanadai kuwa endapo hawatalipwa stahiki zao hizo watagoma mchezo wao wa ijumaa
Na kwamba waliahidiwa wangelipwa fedha zao baada tu ya kuwasili Algeria lakini mpaka juzi suala hilo halikuwepo.
Kiongozi wa timu hiyo, Hakim Serrar alikuwa safarini Algiers kuhudhuria kikao cha viongozi wa klabu, lakini alilazimika kuahirisha safari hiyo baada ya kuona kwenye vyombo vya habari kwamba wachezaji wameanza mgomo.
Kutokana na hilo, shughuli zote za klabu hiyo zilisimama tangu juzi mpaka hapo uamuzi mwingine utakapotolewa na uongozi ulikuwa ukifanya jitihada kuwalipa wachezaji chao.
Hata hivyo, viongozi wana muda mfupi sana kutafuta fedha kwa ajili ya kulipa wachezaji wao kabla ya kukutana na Simba kesho na kama hazitapatikana na wachezaji wakaendelea na
mgomo wao kuna hatari ya kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa kwa miaka miwili.
Hakim Serrar hakufanya siri kulizungumzia hilo kama tatizo kubwa katika historia ya SSE, na pia hakuficha kwamba wachezaji walikuwa na haki ya kufanya uamuzi waliofikia.
Simba iliondoka jijini Jumapili kuelekea Setif itakapochezwa mechi hiyo kesho ambapo kabla ya kuelekea Algeria kwanza walilala Cairo, Misri na Jumanne kuelekea Setif.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment