tuwasiliane

Thursday, April 5, 2012

05 APR.Chini ya kapeti: Yanga warejeshewa point zake


KAMATI ya Niodhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) usiku huu hatimaye imefikia uamuzi wa kuirejeshea klabu ya Yanga pointi zake tatu ilizoponywa na Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom ya Tanzania Bara.

Yanga ilipokonywa pointi hizo kwa kosa la kumtumia beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika mechi dhidi ya Coastal Union, kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga Jumamosi, Coastal ilicheza chini ya pingamizi katika mchezo huo, ambao ilifungwa 1-0 ikipinga klabu hiyo kumtumia beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ikidai alikuwa hajamaliza adhabu yake ya kukosa mechi tatu baada ya kupewa kadi nyekundu kwa vurugu kwenye mechi dhidi ya Azam FC Habari za ndani kutoka kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu zimesema kwamba Yanga wamerejeshewa pointi zao, ingawa kikao hicho bado kinaendelea.

Yanga iliamua kumtumia Cannavaro baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF, Alfred Tibaigana kusitisha adhabu zote zilizotolewa na Kamati ya Ligi kuwafungia wachezaji watano wa Yanga kwa kufanya fujo kwenye mechi na Azam FC, ikiwemo kumpiga refa.

Tibaigana alisitisha adhabu zote akidai kwamba Kamati ya Ligi haina mamlaka ya kutoa adhabu, ispokuwa Kamati yake.

Kwa matokeo hayo, Yanga sasa inarejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 46, baada ya kucheza mechi 21, wakati Azam iliyochezamechi 22 ina pointi 47. Simba inayoongoza ligi hiyo kwa pointi zake 50, nayo imecheza mechi 22, moja zaidi, dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga.

SOURCE ABOOD MSUNI

No comments:

Post a Comment