tuwasiliane

Saturday, March 31, 2012

31 MARCH.VODACOM PREMEIR LEAGUE (VPL)




Ligi kuu ya Vodacom inataraji kuendelea katika viwanja vitatu ambapo Simba, Yanga na Azam watakuwa katika mawindo makali ya kusaka point zote 3.

Yanga watakuwa jijini Tanga kuwakabili vijana wa jiji hilo na mabingwa wa zamani wa Bara Coastal Union, wakati wapinzani wao wa jadi Simba wakikwaana na African lyon, huku Azam wakipepetana na JKT RUVU.

AFRICAN LYON Vs SIMBA SC
Mpambano huu utapigwa leo (machi 31) katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa 10 kamili alasiri.

African Lyon iko katika hatari ya kushuka daraja hivyo point 3 hizo ni muhimu kwao kama ilivyo kwa Simba wanao taka kurejesha ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom katika mtaa wa Msimbazi.

Simba watashuka katika mchezo huo wakiwa na morali mkubwa baada ya Ushindi walioupata kwa waarabu Es-setif mwishoni mwajuma lililopita na kuwepo kwa taarifa ya kupewa haki yao.

COASTAL UNION Vs YANGA
Mchezo huu unatazamwa kuwa mchezo wa juma na utachezwa leo (machi 31) katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Ugumu wa mchezo huo unakuja kutokana na taarifa zilizoenea ya kwamba Coastal Union imeingia ubia na Azam na Simba kwa ajili ya mchezo huo mmoja, na hao ndio wapinzani wa kubwa ya yanga katika kuelekea ubingwa.

Yanga wanaweza wakawatumia wachezaji wake watano waliofungiwa ambao ni Jerry Tegete, Nadir Haroub 'Cannavaro', Nurdin Bakari, Omega Seme na Stephan Mwasika.

AZAM FC Vs JKT RUVU
Mtanange huo utachezwa kesho katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi jijini Dar es Salaam .

Timu zote mbili zinasifika kwa mpira wa pasi nyingi, na mshindi wa michezo yao huamuliwa na uimara wa sehemu ya kiungo kwa timu hizo katika siku hiyo ya mchezo.

No comments:

Post a Comment