
Mwenyekiti wa Simba SC Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa hakuna mgomo wowote ndani ya timu yake ya Simba kama vyombo vya habari vilivyo ripoti hapo awali.
Kuna taarifa zilienea kuwa hali ndani ya timu ya Simba SC si shwali kutokana na wachezaji wa timu hiyo kudai mgao wao wa mchezo wa awali wa raundi ya pili kati ya Simba na ES-Setif uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Rage akizungumza na kituo kimoja cha redio nchini alisema kuwa hawautambui mgomo huo na hali katika kambi ya timu yake iko shwari.
"Taarifa ni za uzushi na wanao zusha hawaitakii mema simba, wachezaji wetu hawana matatizo na wananidhamu nzuri," alisema Rage.
Wakati Rage akisema hayo kunataarifa zimetoka jioni hii, ambazo zinadai kwamba Geofrey Nyange Kaburu amewapa wachezaji wa Simba pesa zao walizokuwa wanazidai.
Kikosi cha Simba SC kiko kambini Bamba Beach wakijiandaa na michezo ya Ligi kuu ya Vodacom na ule wa marejeano wa kombe la Shirikisho dhidi ya Es-setif ya Algeria utakaochezwa kati ya April 6-8.
Katika kambi hiyo kiraka wa timu hiyo Patrick Mutesa Mafisango ameondolewa katika kambi hiyo kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Rage akizungumzi kuondolewa kambini kwa Mafisango amesema kuwa Mafisango hata kuwa nnje ya kikosi kutokana na utovu wa nidhamu alioufanya jana na atasikilizwa baada ya mchezo wa marejeano dhidi ya ES-Setif.
Rage amesema kuwa kwa sasa wanangoja taarifa toka kwa meneja wa timu Nicodas Nyagawa na kocha wa kikosi hicho M4lovan Cirkovic juu ya tukio hilo alilolifanya Mafisango hapo jana.
No comments:
Post a Comment