Mchezaji wa Simba SC kutoka Rwanda mwenye asili ya DR Congo Patrick Mutesa Mafisango ameondolewa kwenye kambi ya Simba SC iliyopo Bamba Beach.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo katika mitandao mbalimbali, Mafisango amerejea kosa lake la ulevi lililopelekea hapo nyuma kuondolewa katika kambi ya timu hiyo.
"Mafisango baada ya kuwa 'tungi' aliporejea kambini alitoa luigha chafu kwa meneja wa timu hiyo Nicodemus Menard Nyagawa pamoja na kocha mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic kabla ya taarifa kufika kwa uongozi na ndipo mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage kuagiza atimuliwe." ilieleza moja ya taarifa toka katika mitandao.
No comments:
Post a Comment