Katika hali isiyokuwa ya kawaida daladala zimeweza kugoma kufanya kazi katika jiji la mwanza
kwa mujibu wa baadhi ya makondaka ambao niliweza kufanya mahojiano nao wamesema sababu kubwa ya wao kuweza kugoma ni kupinga kodi ya shiling 500 ambayo hutuzwa kila wanapoingia katika vituo vya daladala
wanadai kuwa pesa hito ni kubwa kwa wao kwani vitu vingi vimeweza kupanda kwa hiyo hali hiyo inawapelekea wao kupata wakati mgumu sana kukabiliana na maisha
nilpata kufanya mahojiano na bwana Ali seif yeye ni konda anayefanya safari za malimbe-mjini anasema leo wao imewalazimu kutembea kuishia kituo cha tanesco ili kuwakwepa wenzao waliokuwa wakiwarushia mawe pindi tu wafikapo mjini kwani walikuwa wanataka magari yote yagome leo
lakini kufikia muda wa jioni hivi serikali ya jiji la mwanza kupitia kwa mkuu wa mkoa waliweza kuwaomba baadhi ya wafanya biashara kama mukesh vunja bei kuingiza gari zao barabarani ili kusaidia kuondoa tatizo hilo
hadi narudi chuo ilinilazimu kupanda escudo kutoka mjini kwa shilingi 1000
ndio tanzania ya leo hiyo kila kitu mgomo
No comments:
Post a Comment