tuwasiliane

Sunday, March 25, 2012

25 MARCH. SIMBA YAFANYA KWELI




Magoli yaliyofungwa na wachezaji wa simba toka Uganda na Zambia, Emanuel Okwi na Felix Sunzu yalitosha kuwapatia ushindi Simba SC wa goli 2-0 dhidi ya Es-setif ya Algera mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa.

Sunzu na Okwi waliwatoa kifua mbele Simba katika mchezo wa pili wa raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho dhidi ya Kiyovu katika uwanja wa Taifa na leo kurudia kitendo hicho.

Katika mchezo wa leo Emanuel Okwi akuonyesha makali yake katika kipindi cha kwanza ambapo Simba walimsimamisha mshambuliaji mmoja Felixs Sunzu.


Simba walitawala mchezo katika vipindi vyote vya mchezo na ilibidi wangoje mpaka dakika ya 75 kupata goli la kuongoza kupitia kwa Emanuel Okwi.


Simba SC waliandika goli la pili kupitia kwa Felixs Sunzu ambapo aliunga mpira uliotemwa na kipa wa ES Setif ambao walicheza bila ya washambuliaji wao wa kutumainiwa wa wawili. Kipa huyo aliutema mpira huo kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Salum Machaku katika dakika ya 80.

Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa Simba 2-0 ES-Setif. Kwa matokeo hayo ES-Setif watakuwa na kibarua cha kusaka goli 3-0 ili wasonge mbele katika hatua inayofuata hapo April 6, mchezo utakao chezwa nchini Algeria.

No comments:

Post a Comment