tuwasiliane

Saturday, March 24, 2012

24 MARCH.TP Mazembe, Esperance, Al Ahly zaingia vitani


VIGOGO Afrika wanashuka dimbani leo na kesho katika harakati zao za kusaka ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika 2012.Mabingwa watetezi Esperance wataanza kampeni yao ya kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi kwa kucheza dhidi ya Brikama United ya Gambia, wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa wameshinda mechi nane za ligi ya kwao na wakiwa katika kiwango kizuri.

Itakuwa ni jambo la kushangaza kama watashindwa kupata matokeo mazuri hapo, lakini watakuwa na nafasi ya kujirekebisha watarudiani jijini Tunis.

Mabingwa wa Afrika mara mbili 2009 -10, TP Mazembe wenyewe watakuwa ugenini nchini Zambia kuwavaa Power Dynamos kwenye mchezo unaotegeme kuwa na upinzani mkubwa.

Mazembe walifungiwa kucheza mashindano hayo msimu uliopita kwa kumchezesha mchezaji asiyekuwa wa kwao, kwa lengo la kutafuta ubingwa wa tatu mfululizo.

Wanajua mchezo dhidi ya Power Dynamos utakuwa na ugumu wa kipekee, japokuwa Mazembe imeundwa na wachezaji wengi kutoka Zambia.

Vigogo wa Mirsi, Al Ahly watacheza mechi ya kwanza tangu walipokumbwa na balaa la Port Said lilisabisha kupoteza maisha ya watu 74 kutokana na vurugu za mashabiki kwenye mchezo dhidi ya Al Masri. Watakuwa jijini Addis Ababa kucheza na Coffee ya Ethiopia huku wakipewa nafasi kubwa ya kushinda.

Lakini kusimamishwa kwa Ligi ya Misri kuna maanisha wanaingiwa uwanjani bila ya kucheza mechi yoyote ya ushindani, japokuwa wachezaji wamedai watapigana kwa ajili ya kocha wao Manuel Jose.

Mabingwa wa Nigeria, Dolphins watakuwa na kibarua nchini Cameroon kuivaa CotonSport mchezo unategemewa kuwa na uzuri wa kipekee kwa timu hizo mbili kusaka kuingia hatua ya makundi.

Mchezo mwingine Zamalek watakuwa na kibarua dhidi ya Africa Sports, huku mabingwa wa Sudan, Al Hilal watakuwa ugenini dhidi ya DFC8 ya Jamhuri ya Afrika Kati, nao vijogoo wa Ghana, Berekum Chelsea watawaburushisha Raja Casablanca ya Morocco.

Wafalme wa Angola, Recreativo Libolo watakuwa wenyeji wa Sunshine Stars ya Nigeria.

No comments:

Post a Comment