tuwasiliane

Saturday, March 24, 2012

24 MARCH.LADY JAY DEE AINGIZA ALBUM YAKE YA TANO KITAA


MWANAMUZI Judith Wambura a.k.a 'Lady Jay dee', Mama Somefood, Komandoo, Binti Machozi na majina mengine kedekede,ameingiza sokoni albamu yake aliyoipa jina ya Tano, Best of Lady Jay Dee.

Albamu hiyo ambayo ni 'makusanyo' ya nyimbo alizoimba tangu mwaka 2000 na za sasa kiasi, aliingiza sokoni mwishoni mwa wiki.

Jide alisema ameamua kuingiza sokoni albamu hiyo yenye nyimbo 25 baada ya mashabiki wake kuulizia sana nyimbo zake za zamani.

Alisema kwa kuwa nia yake ni kuwafurahisha na kuwaburudisha wasikilizaji na wapenzi wa bendi ya Machozi ameamua kuwaandalia 'Collection' hiyo ambayo ipo sokoni kwa sasa.

"Nilipata maombi mengi kutoka kwa mashabiki wangu wakitaka kusikia nyimbo zangu za zamani ,nikaamua kuandaa 'collection' hii kwa kuwawekea za zamani na za sasa kidogo "alisema Jide.

Anasema mkusanyiko huo ni kutoka katika albamu zake zote ambazo ni Asubuhi ya 2000, Machozi, Binti, Moto, Shukrani na baadhi mpya ambazo hazijawahi kusikika.

No comments:

Post a Comment