tuwasiliane

Wednesday, March 21, 2012

21 MARCH.Mkwasa aita 25 Twiga Stars


KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha wachezaji 25 kitakachoingia kambini Machi 25 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya
programu yake ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Ethiopia.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema jana kuwa
wachezaji walioitwa kambini na timu zao katika mabano ni Amina Salum (Lord Baden Sekondari, Pwani), Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (New Generation, Zanzibar) na Esther Mayala (Street Girls, Mwanza).

Wengine ni Evelyn Senkubo (Mburahati Queens), Fadhila Hamad (Uzuri Queens) na Fatuma
Bashiri (Simba Queens), Fatuma Gotagota (Mburahati Queens) na Fatuma Khatib (Mburahati
Queens).

Pia wapo Fatuma Mustafa (Sayari), Fatuma Omari (Sayari), Hanifa Idd (Uzuri Queens),
Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (JKT), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens) na
Mwanaidi Khamis (Uzuri Queens).

Wambura aliwataja wengine kuwa ni Mwapewa Mtumwa (Temeke), Rukia Khamis (Sayari),
Semeni Abeid (Tanzanite), Siajabu Hassan (Evergreen), Tatu Salum (Makongo Sekondari), Upendo Jeremiah (Pangani, Tanga), Veneranda Mbano (Tanzanite), Zena Khamis (Mburahati
Queens) na Zena Said (Uzuri Queens).

No comments:

Post a Comment