tuwasiliane

Tuesday, March 20, 2012

20 MARCH. Machupa apata timu mpya



MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba SC na Malindi ya Zanzibar, Athumani Machupa amejiunga na klabu ya Vasby United ya Daraja la Kwanza Sweden akitokea Vasalund ya Daraja la Pili.

Machupa ameiambia bongstarz dakika kadhaa zilizopita kwamba alilazimika kufanya majaribio kwenye timu hiyo na baada ya kufuzu ndipo akapewa mkataba wa miaka mitatu.

"Maisha yanaendelea ndugu yangu, mkataba mzuri namshukuru Mungu, kinachofuata hapa ni kazi tu, naamini unaniaminia jembe lako, wewe subiri tu kuandika mabao nayofunga huku, nina ari mpya na nguvu mpya," alisema Machupa.

Source: Bin Zubeir

No comments:

Post a Comment