tuwasiliane

Saturday, March 10, 2012

10 MARCH.YANGA 1 AZAM 3



Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu ya Vodacom, Yanga leo wamefungwa na Azam FC goli 3-1 wakiwa pungufu kwa wachezaji wawili walio limwa kadi nyekundu.

Katika mchezo huo wa Ligi kuu ya Vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa, Azam walianza kuhesabu magoli katika dakika ya 4 kufuatia goli la Mshambuliaji hatari wa Azam John Bocco Adbayor.

Goli hilo la mapema liliwashtua Yanga na katika dakika ya 12 na 14 walishuhudia kiungo wa kimataifa toka Rwanda Haruna Niyonzima na beki Nadir Haroub walizawadiwa kadi nyekundu, ikiwa ni kadi ya pili za njano kwao.

Kadi nyekundu hizo zilimpelekea kocha wa Yanga Kostadin Papic kufanya mabadiliko kwa kumtoa Davis Mwape na Kuingia Chacha Marwa na dakika ya 24 alimtoa Shamte Ally na kuingia Godfrey Bonny.

Yanga walirejea mchezoni baada ya goli la Hamisi Kiiza katika dakika ya 30 na kupelekea mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko kwa upande wa Azam FC ambapo AbdiKasim 'Babi' alichukua nafasi ya Ibrahim Mwaipopo. Na katika dakika ya 54 kiungo toka Ivory Coast Michael Bolou alifunga goli lake la kwanza katika ligi kuu ya Vodacom na kuipa uongozi wa goli 2-1.

John Bocco alirudi tena nyavuni katika dakika ya 76 na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kushinda goli 3-1.

Kwa ushindi wa leo Azam wamekaa kileleni kwa mda uku wakivunja rikodi zake kwa kufikisha point 41 na kuwa mchezo wa 4 kuifunga Yanga mfululizo.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Azam FC (20) 41
2. Simba SC (18) 40
3. Yanga SC (18) 37
4. Mtibwa Sugar (20) 34
5. JKT Oljoro (21) 28
6. JKT Ruvu (20) 27
7. Coastal Union (20) 26
8. Kagera Sugar (20) 24
9. Ruvu Shooting (20) 24
10. African Lyon (17) 18
11. Moro United (21) 18
12. Villa Squad (19) 16
13. Toto Africa (19) 16
14. Polisi Dodoma (19) 14

No comments:

Post a Comment