tuwasiliane

Saturday, March 10, 2012

10 MARCH. Afande na DONGO kwa WATANGAZAJI!


Toka mji kasoro bahari 'Morogoro' msanii Seleman Msindi ‘Afande Sele’, amerusha dongo kwa watangazaji na ma-Dj wa vituo vya redio na televisheni kuacha tabia ya kuzibeba na kuzipiga nyimbo kutoka kwa wasanii wa nje, badala yake wafanye hivyo kwa wasanii wa nyumbani.

Afande anadai vyombo vya habari vimekuwa na utamaduni wa kupiga nyimbo za nje badala ya za ndani na kuvitaja kama mhimili wa kudumaa kwa sanaa hiyo na wasanii kwa ujumla.

Hata hivyo alikiri kuwa kwa namna moja wasanii nao ni kikwazo kwa maendeleo ya muziki, kwani mwanzo walikuwa wanaumiza vichwa na kutunga mashairi yanayoelimisha jamii, tofauti na sasa, kwani muziki ni mwepesi na hivyo kusababisha kutokupiga hatua na kuendelea mbele, kutokana na kuwa na ladha isiyo ya kiasili.

No comments:

Post a Comment