Tuesday, March 6, 2012
06 MARCH.Simba kuweka Kambi Ufaransa
VINARA wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC inatarajia kuweka kambi kwa muda wa siku tano nchini Ufaransa ili kujiwinda na wapinzani wao timu ya Es Setif ya Algeria katika raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho ambapo wataanzia ugenini Machi 23-25.
Hayo yalisemwa jana na Ismail Aden Rage alipoojiwa na moja ya Redio (redio Uhuru) hapa alipoulizwa juu ya maandalizi yao kufuatia kuwatoa Kiyovu kwenye kombe hilo la washindi.
Rage alisema wanaanza mchakato huo mara moja ilikuona wanaua kwenye mazingira mazuri na kukabiliana na wapinzani wao hao.
"Kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kuona timu inaweka kambi ambayo itazaa matunda na tunafikilia kuweka nchini Ufaransa ambayo itakua kwa siku tano na baadae kuingia moja kwa moja nchini ALGERIA" alisema Rage.
Rage alisema watakutana na viongozi muda mchache kufuatia kuisha kwa mechi hiyo na leo ilikuona wanapanga mikakati ya ushindi ilikushinda mchezo huo wa ugenini baada ya hapo kuelekea kwenye hatua nzuri.
Aidha, Rage aliwapongeza mshabiki wa Simba na Yanga kujitokeza kuishangilia Simba kwa amani na utulivu huku akiwapongeza Yanga kwa kuonyesha Uzalendo wa kuishangilia Simba na kutovaa jezi za Kiyovu.
"Nawapongeza mashabiki wa Yanga kwa kutuunga mkono na kuonyesha Uzalendo, hii ndio inayotakiwa kwenye soka" alisema Rage.
"Jinsi gani timu inajiandaa vizuri na kua kwenye wakati salama ikiwemo kuweka kambi ya uhakika nje ya nchi, na nchi ya Ufaransa itakua ni nzuri kwetu kwani mzingira yake yatasaidia kwani tulishawai kuweka kambi nchi hiyo huko nyuma na sasa tunatarajia kuweka tena" alisema Rage juu ya mkakati wao wa kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Simba wamefika katika hatua hiyo kufuatia ushindi wa goli 2-1 walioupata jana mbele ya Kiyovu ya Rwanda katika uwanja wa Taifa, hivyo Simba kuwaondoa Kiyovu katika mashindano ya kombe la shirikisho CAF kwa jumla ya goli 3-2 kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa awali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment