tuwasiliane

Friday, March 2, 2012

02 MARCH.JOHN BOKO;WATANZANIA MNISAMEHE


MSHAMBULIAJI wa Azam na Taifa Stars, John Boko amesema hakuwa na bahati ya kufunga katika mchezo dhidi ya Msumbiji na amewaomba radhi mashabiki na kudai ni makosa ya kibinadamu na humkuta mchezaji yeyote duniani.

Kutokana na kukosa nafasi nyingi kwenye mchezo huo kinara huyo wa ufungaji wa Ligi Kuu aligeuka gumzo miongoni mwa watazamaji waliofika kushuhudia pambano hilo juzi.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo Boko alisema ni wazi alipoteza nafasi nyingi za kufunga alizopata, lakini lazima mashabiki wafahamu makosa ni sehemu ya mchezo.

"Ni makosa ya kawaida sana kukosa goli hata nchi za wenzetu hali ni kama hii, nimekosa magoli ya wazi nakubali, lakini mashabiki wasione huu ni mwisho bado tunaweza kushinda na kusonga mbele katika mashindano hayo," alisema Boko.

No comments:

Post a Comment