
Imegundulika kuwa midume mingi iliyo kwenye ndoa na ambao wameamua kujitokeza kufanyiwa tohara, hawafanyi hivyo kwa maamuzi yao bali ni kwa ushauri na ushawishi wa wake zao.
Uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo kwa mkoa wa Rukwa, Sumbawanga tangu Januari mwaka jana, vijana wenye umri wa kati ya miaka 14 na 23 mjini hapa, ndio waliokuwa wakiongoza kwa wingi kutahiriwa.
Lakini sasa wanandoa wenye umri kati ya miaka 25 had 75 wamehamasika na kujitokeza kwa wingi kufanyiwa tohara hiyo kwa hiyari yao wenyewe kwa maelezo kwamba wameshawishika kufanya tohara hiyo baada ya kuhamasishwa na wake zao.
Meneja Mradi wa Nyanda za Juu Kusini, Dk. Zegeli Bilishanga alisema kuwa mwanandoa aliyevunja rekodi ya umri mkubwa aliyemtahiri hivi karibuni katika Hospitali hiyo ya Mkoa mjini Sumbawanga alikuwa na umri wa miaka 75.
“Kabla ya kumtahiri mzee huyo mwenye umri wa miaka 75, nilimuuliza amesikia wapi na kwa nani kuwa hospitalini hapa kunafanyika tohara ya wanaume… kwa furaha kubwa alinieleza kuwa amehamasishwa na mkewe kufanya tohara hiyo ya wanaume.
No comments:
Post a Comment