tuwasiliane

Thursday, February 16, 2012

16 FEB. Simba kupaa Kigali leo


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuno ya Kombe la Shirikisho, Simba ya jijini Dar es Salaam, inaondoka leo jioni kwenda Rwanda tayari kwa mechi ya Jumamosi wiki hii dhidi ya wenyeji wao Kiyovu ya jijini Kigali.

Msafara wa Simba unataraji kuwa na watu 40 na watarejea Jumapili mara baada ya mchezo.
Kocha Curkovic Milovan atatangaza majina ya wachezaji wataokwenda safari hiyo leo kwa usafiri wa ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda.

Wakizungumza mara baada ya mazoezi yao ya jana asubuhi wachezaji, wachezaji wa vinara hao wa Ligi Kuu Bara wamesema wana matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo.

Kipa Juma Kaseja alisema wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo kutokana na maandalizi mazuri waliyofanya mpaka sasa.

"Ni kama vita, tunakwenda kupambanana tukiwa na matumaini tele. Tunaomba mashabiki wetu watuunge mkono na kutuombea," alisema Kaseja.

Kauli ya Kaseja iliungwa mkono na ile ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi aliyesema wanakwenda kusaka ushindi ugenini ili mechi ya marudiano iwe rahisi nyumbani.

Naye iungo Mwinyi Kazimoto alisema mashabiki wa Simba watarajie mazuri kwenye mechi hiyo kwani wanakwenda kucheza kufa na kupona ili wapate ushindi.

No comments:

Post a Comment