tuwasiliane

Sunday, February 12, 2012

12 FEB.Yanga washinda na kurejea Kileleni



Mabingwa wa Tanzania Bara Young African Sports Club (yanga) wameendeleza sherehe yao ya kufikisha miaka 77 toka ianzishwa katika uwanja wa Taifa baada ya kuchukua point 3 muhimu na kurejea katika nafasi ya kwanza.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom ulioanza saa kumi na nusu alasiri Yanga wameibuka na ushindi wa goli moja bila lililopatikana katika kipindi cha pili kupitia kwa Davis Mwape katika dakika ya 46.

Katika kipindi cha kwanza Yanga walipoteza penati iliyopigwa na Hamisi Kiiza kufuatia kuangushwa kwa Davis Mwape katika eneo la hatari.

MSIMAMO WA VPL.
Kwenye Mabano Idadi ya Mechi Zilizochezwa.
1. Yanga SC (17) 37
2. Simba SC (17) 37
3. Azam FC (17) 32
4. JKT Oljoro (17) 26
5. JKT Ruvu (17) 23
6. Mtibwa Sugar (16) 22
7. Kagera Sugar (16) 20
8. Coastal Union (17) 20
9. Ruvu Shooting (17) 18
10. African Lyon (16) 17
11. Villa Squad (17) 16
12. Moro United (17) 16
13. Toto Africa (16) 14
14. Polisi Dodoma (17) 13

No comments:

Post a Comment